Wapelelezi katika Kaunti ya Bungoma wanachunguza wizi wa mchana ambapo familia moja ilivamiwa na wanaume sita wenye silaha na kuibiwa zaidi ya Sh500,000 pesa taslimu na vitu kadhaa vya thamani kando ya Barabara ya Chwele-Lwakhakha. Tukio hilo lilitokea yapata saa sita unusu mchana Jumanne karibu na Daraja la Ndakaru katika Kaunti Ndogo ya Bungoma Magharibi. Polisi wanashuku washambuliaji walikuwa na taarifa za awali kuhusu miamala na mienendo ya familia hiyo.