Seneti leo itazindua Kielezo cha Upimaji wa Utendaji wa Fedha za Kaunti, chombo cha kisayansi kilichotengenezwa ili kutathmini jinsi serikali za kaunti zinavyosimamia rasilimali za umma. Spika Amason Kingi anasema kielezo hicho, kilichoandaliwa na Ofisi ya Bajeti ya Bunge, kitapima kaunti kwa viashiria muhimu vya fedha za umma ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa bajeti, matumizi ya maendeleo na matokeo ya ukaguzi. Seneti inasema chombo hicho kitaimarisha usimamizi wa fedha zilizogatuliwa na kukuza uwazi, uwajibikaji na utoaji huduma ulioboreshwa katika kaunti zote.
AMASON KINGI – INDEX