Kampuni ya Nairobi Water inaweza kuhitajika kuunda mpango kamili wa uboreshaji wa maji na usafi wa mazingira ikiwa Seneti itapitisha hoja ya Seneta Mteule Catherine Mumma. Pendekezo hilo linalenga kupanua upatikanaji wa maji safi na usafi wa mazingira katika makaazi yasiyo rasmi kupitia malengo na ratiba zilizo wazi. Pia linatoa wito wa kuimarishwa kwa miundombinu ya usambazaji wa maji, kupanua mitandao ya maji taka na utoaji wa huduma kwa bei nafuu kwa wakaazi wa Nairobi.
CATHERINE MUMMA – NAIROBI