Waziri wa Afya Aden Duale anasema mageuzi yanayoendelea ya huduma za afya yamepanua upatikanaji wa CT scans, mammography, vyumba vya upasuaji na huduma za maabara kote nchini. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Huduma ya Dharura ya SHA 922, Waziri Duale alisema KEMSA sasa inasambaza bidhaa tisa kati ya 10 za matibabu zinazoombwa, huku serikali ikiwa imeajiri wauguzi na wakunga 5,000 na imejipanga kuanzisha Kituo cha Kitaifa cha Uratibu wa Ambulensi.
ADEN DUALE – HEALTH REFORMS