Kura ya maoni ya hivi karibuni ya Infotrak imezua mjadala kuhusu utendaji wa ugatuzi katika sekta ya afya. Naibu Katibu Mkuu wa KMPDU Dennis Miskellah anasema ni jambo la kutiliwa shaka kuwapa baadhi ya magavana sifa kubwa wakati kaunti nyingi zimejenga hospitali na kununua vifaa bila kuajiri wafanyakazi wa kutosha wa afya. Kura hiyo iliipa elimu, mazingira, na uhandisi alama kama baadhi ya sekta zinazofanya vizuri zaidi chini ya ugatuzi huku sekta ya afya ikiwa haikuonekana popote kwenye orodha.
DENNIS MISKELLAH – DEVOLUTION