Kaunti ya Kirinyaga imesifiwa kwa maendeleo yake katika kubadilisha ufugaji wa samaki kuwa biashara yenye faida. Gavana Anne Waiguru alisema kaunti hiyo imebadilisha kimakusudi ufugaji wa samaki kutoka shughuli ya kujikimu hadi mnyororo wa thamani unaofaa kibiashara ukiwa na uzalishaji wa sasa wa tani 71.3 na lengo la kila mwaka la tani 400. Alisema kuwa utawala wake umekuwa ukiunga mkono maendeleo ya ufugaji wa samaki katika kaunti hiyo kupitia utoaji wa viunga vya mabwawa ya samaki, samaki wadogo , chakula cha samaki na huduma za nyanjani.
ANNE WAIGURU – FISH FARMING