Seneta wa Taita Taveta Johnes Mwaruma amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Umma na Uwekezaji ya Kaunti, ya Seneti. Mwaruma alichaguliwa kwa kauli moja kuchukua nafasi ya seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi ambaye amekuwa mwenyekiti wa jopo hilo tangu mwaka 2022. Seneta mteule Beth Syengo pia amechaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa jopo hilo, akichukua nafasi ya seneta wa Migori Eddy Oketch ambaye aliondolewa kwenye jopo hilo katika mabadiliko yaliyoidhinishwa na Bunge mapema wiki hii.