Mwenyekiti wa Baraza la Magavana Ahmed Abdullahi amewasihi magavana kuacha kukosoa hadharani Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA) na badala yake wafanye kazi kwa karibu na shirika hilo ili kutatua changamoto zinazoathiri huduma za afya. Abdullahi anasema magavana wanapaswa kuwasiliana na SHA moja kwa moja wakati wowote kunapotokea ucheleweshaji wa utoaji wa madai. Alisisitiza kwamba bima hiyo ya matibabu inafanya kazi, ina ufanisi, na ina uwezo wa kutoa huduma bora za afya kote nchini.
AHMED ABDULLAHI –SHA