Viongozi wa dini ya Kiislamu wameipongeza serikali ya Kenya Kwanza kwa kufuta mchakato wa zaidi ya miaka 60 wa kuwachunguza waombaji wa vitambulisho vya taifa kutoka jamii ya Waislamu na wakaazi wa Kaskazini mwa Kenya na kaunti za mpakani. Wakizungumza katika Ikulu, viongozi hao pia walimpongeza Rais kwa kuunga mkono ujenzi wa misikiti, madrasa, na vituo vingine vya kidini. Pia waliihimiza serikali kuongeza idadi ya walimu wa elimu ya dini ya Kiislamu katika shule za umma.


VOX POP-SCRAP