Rais wa FKF, Hussein Mohammed, anasema watajijenga upya ili kuhakikisha matokeo bora baada ya Harambe Starlets kufanya vibaya katika mashindano ya WAFCON jana usiku. Hata hivyo, msimamizi huyo mzoefu wa soka anaamini wamejifunza masomo muhimu, baada ya kurudi kwenye mashindano hayo ya bara baada ya miaka 10. Starlets walipoteza 2-0 dhidi ya Algeria katika pambano la mwisho la kundi A, kupoteza kwao kwa mara ya tatu mfululizo na kumaliza chini bila pointi.
HUSSEIN MOHAMMED - STARLETS
Msururu wa LOOP Gravel Safari mwaka 2026 unaelekea Pwani baadaye mwezi huu huku awamu ya tatu ya msururu huo ikipangwa tarehe 29 mwezi huu huko Vipingo Ridge katika Kaunti ya Kilifi. Kufuatia raundi mbili zilizofanikiwa huko Limuru na Naivasha, msururu huo sasa unaelekea Kilifi, ambapo zaidi ya waendesha baiskeli 500 wanatarajiwa kushindana katika kategoria za mbio za kilomita 30, kilomita 55 na kilomita 105. Timu itakayoshinda itapata shilingi 125,000 huku timu za pili na tatu zikipokea shilingi 100,000 na shilingi 70,000, mtawalia.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi, Narok na Kajiado.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.