Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna ametoa wito wa uwazi zaidi katika usimamizi wa mfumo wa SHA ili kuongeza uwajibikaji na kurejesha imani ya umma katika mpango huo mpya wa bima ya afya. Seneta Sifuna alionya kwamba ukosefu wa uwazi unaweza kudhoofisha uaminifu wa umma na ufanisi wa mpango huo. Alihimiza serikali kuweka kipaumbele mageuzi yenye maana katika sekta ya afya ili kuhakikisha mfumo wa SHA unatoa huduma bora za afya na zinazopatikana kwa urahisi.
EDWIN SIFUNA –SHA