Katibu wa usalama Raymond Omollo amepongeza uamuzi wa serikali wa kuanzisha malipo ya kila mwezi kwa wazee wa vijiji, akiuelezea kama hatua ya kihistoria katika kutambua jukumu lao katika utawala wa mashinani. Omollo alisema malipo ya awali ya mwezi uliopita tayari yametolewa, na kuifanya kuwa mara ya kwanza wazee wa kijiji kulipwa rasmi kwa huduma yao. Alisema wazee hao wana jukumu muhimu katika kukuza amani, kusuluhisha mizozo na kuunganisha jamii na serikali.

RAYMOND OMOLLO – ELDERS