Wabunge wamehimizwa kuimarisha usimamizi na kuhakikisha mabilioni ya pesa zilizotengwa kwa kaunti zinatumika kwa busara. Mbunge wa Bumula, Jack Wamboka, aliwashutumu baadhi ya magavana kwa kushindwa kuboresha utoaji wa huduma licha ya kupokea ufadhili mkubwa kutoka kwa serikali ya kitaifa. Alitoa wito wa uwajibikaji na uwazi zaidi katika matumizi ya rasilimali za umma ili kuhakikisha walipa kodi wanapata thamani ya pesa na kaunti zinatoa huduma muhimu kwa ufanisi.



JACK WAMBOKA – ACCOUNTABILITY