Wizara ya Elimu imeongeza hatua za kupunguza vurugu shuleni kufuatia wimbi la mashambulizi ya uchomaji shule kote nchini. Akiwa mbele ya wabunge, Katibu wa Elimu John Ololtuaa alisema serikali imeimarisha ushirikiano na bodi za usimamizi na mashirika ya usalama, na kupanua programu za mwongozo na usaidizi wa kisaikolojia. Wazazi, viongozi wa kidini na wasimamizi wa mitaa pia wanashirikishwa ili kusaidia kurejesha nidhamu na kuboresha usalama shuleni.
JOHN OLOLTUAA – MEASURES