Spika wa Seneti Amason Kingi amemkosoa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kwa madai kwamba anaunga mkono juhudi za kumng'oa madarakani Rais William Ruto katika Uchaguzi Mkuu wa 2027. Kingi alisema Uhuru alikuwa amekamilisha mihula yake miwili iliyoamriwa kikatiba na akamtuhumu kwa kutosaidia eneo la Pwani, akitoa mfano wa uhamisho wa baadhi ya shughuli za bandari kutoka Mombasa wakati wa utawala wake. Alimsihi rais huyo wa zamani aruhusu serikali ya sasa kutawala.

AMASON KINGI – UHURU