Baada ya mikondo miwili ya raundi sita ya Sport Pesa National Sevens Circuit, mashindano hayo yanachukua mapumziko ya wiki moja kabla ya kurejea na Kabeberi 7s mnamo Agosti 15-16 jijini Nairobi. Baada ya kushinda Dala Sevens mjini Kisumu kwa 19-5 dhidi ya Menengai Oilers wikendi iliyopita Kabras Sugar RFC ilipanda hadi kileleni mwa jedwali. Kabras inaongoza kwa pointi 41, ikiwa mbele ya mabingwa watetezi KCB RFC walioshinda Prinsceloo7's. Washindi wataenda nyumbani na ksh 150,000 kama zawadi ya pesa taslimu kwa hisani ya sportpesa.



Real Madrid wametoa ofa ya mkataba ulioboreshwa kwa Vinícius Júnior tangu Kombe la Dunia, baada ya kuanza tena mazungumzo ambayo yalikuwa yamesimama kwa karibu mwaka mmoja. Mkataba wa Vinícius wa sasa unaisha Juni 2027 huku uvumi ukiongezeka kuhusu mustakabali wake hivi karibuni, kufuatia kunyatiwa na mabingwa wa Ligi Kuu Arsenal. Madrid sasa wamempa Mbrazil huyo mkataba wenye thamani ya takriban dola milioni 25 kwa mwaka, ongezeko la kile ambacho klabu hiyo ilikuwa tayari kutoa katika mazungumzo katika misimu miwili iliyopita ikisubiri sheria na masharti.



Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi, Narok na Kajiado.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.