Gor Mahia itakabiliana na wenyeji Rayon sport katika fainali za CECAFA 2026 jijini Kigali, Rwanda Ijumaa, baada ya kuwashinda Al-Hilal ya Sudan kwa penalti 8-7, kufuatia sare ya 1-1 katika muda wa ziada. KO'gallo ilichukua uongozi kupitia bao la kujifunga la Steven Ebuela dakika ya 34, kabla ya Sudan kusawazisha kupitia Ansumana Samura na kupeleka mechi katika muda wa ziada. Wakati huo huo, Rayon iliishinda Jamus FC ya Sudan Kusini kwa mabao 3-1 katika mechi nyingine ya nusu fainali. Rayon iliishinda Gor 2-0 katika mechi ya kirafiki mwezi uliopita kabla tu ya cecafa kuanza.

 

Rais wa FIFA anayekumbwa na shinikizo Gianni Infantino amewaita viongozi wakuu wa baraza linaloongoza la soka duniani kwa mkutano nchini Morocco leo. Hii inakuja huku Infantino akikabiliwa na ukosoaji mkali wa mpango wake wa kuuza shughuli za kibiashara na matukio za Fifa. Mkuu wa maendeleo ya soka duniani wa Fifa Arsene Wenger, katibu mkuu Mattias Grafstrom, na rais wa Chama cha Soka cha Jordan, wote waliweka wazi kupinga kwao Fifa Forward Enterprise ya Infantino. Infantino, ambaye amekuwa Morocco wiki iliyopita, anatafuta suluhisho la utata huo.

Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.