Kiungo wa Gor Mahia, Alpha Onyango, atakosa mechi yao ya nusu fainali ya CECAFA dhidi ya Al Hilal Ondurman ya Sudan katika Uwanja wa Kigali Pele, baada ya rufaa yake ya kadi nyekundu kukataliwa. Hata hivyo, kocha mkuu wa KO’gallo, Charles Akannor, anasema wana wachezaji wa kutosha kuchukua nafasi yake wanapotafuta njia ya kuingia fainali kwa mara ya kwanza katika zaidi ya miaka 40. Mechi hiyo itaanza saa kumi jioni kabla ya kutoa nafasi kwa timu ya Jamus FC ya Sudan Kusini dhidi ya Rayon sport. Washindi watapata dola 30,000. Huyu hapa Akannor.



Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Machakos, Kibwezi na Kitui.

Ili kupata habari ziadi tembelea tovuti ya radiojambo.