Mbunge wa Mukurwe-ini John Kaguchia anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo kufuatia kukamatwa kwake kuhusu madai ya kusambazwa kwa video ambapo inasemekana alitoa matamshi tata akiwalenga wafuasi wa Rais William Ruto. Wakili wake, Ndegwa Njiru, amelaani jinsi DCI ilivyoshughulikia kukamatwa huko, akidai timu ya mawakili ya mbunge huyo ilinyimwa nafasi ya kumfikia mteja wao na kuzuiwa kuwasiliana naye.

NDEGWA NJIRU – KAGUCHIA