Mahakama ya Hakimu Mkaazi ya Milimani leo inatarajiwa kutoa maelekezo kuhusu kujibu mashtaka kwa Mbunge wa Mukurwe-ini, John Kaguchia. Mahakama iliahirisha kikao jana baada ya mbunge huyo kuondoka katika majengo ya mahakama kinyume na agizo lake, na kuvuruga kesi. Kaguchia anakabiliwa na shtaka la kufanya uhalifu unaosababisha kuvunjika kwa amani. Aliachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu ya shilingi 250,000 au bondi ya shilingi milioni 1 akisubiri kesi.

TERESIA NYANGENA –RELEASE