Maafisa wa chama cha wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Nairobi wameonya kwamba sera iliyopendekezwa ya kustaafu inaweza kuvuruga shughuli za taasisi hiyo kwa kiasi kikubwa, wakibaini kuwa karibu asilimia 40 ya wafanyakazi wake wa kitaaluma wanakaribia umri wa kustaafu. Wakiongozwa na Profesa George Osanjo, maafisa hao walionya kwamba kutekeleza sera hiyo kunaweza kulemaza idara na taaluma zote kutokana na uhaba wa wahadhiri wenye uzoefu. Sera hiyo inapunguza umri wa kustaafu kwa maprofesa kutoka miaka 74 hadi 70 na kwa wahadhiri wakuu na wafanyakazi wengine wa kitaaluma kutoka miaka 74 hadi miaka 65 na chini.

VOX POP – WARNING