Bunge la Kitaifa limepitisha Muswada wa Mgao wa Ziada wa Serikali za Kaunti, 2026, unaofungua njia ya ufadhili wa ziada kwa kaunti katika mwaka wa fedha wa 2026/27. Mswada huo unatoa rasilimali za ziada ili kuimarisha utoaji wa huduma na kuharakisha miradi ya maendeleo katika kaunti zote. Mgao mkubwa zaidi, Sh bilioni 8.61, utasaidia mpito wa wafanyakazi wa UHC hadi masharti ya kudumu na ya pensheni, huku pia ukitoa ufadhili wa ziada kwa wakuzaji afya wa jamii ili kuongeza huduma za afya mashinani.

VOX POP – APPROVE