Kabras Sugar RFC iliwashinda Menengai Oilers 26-5 na kushinda Msururu wa kitaifa wa sevens wa SportPesa, katika Dala7'S katika Uwanja wa Mamboleo, mjini Kisumu jana. John Okoth aliwaweka Oilers mbele kwa try ya mapema, lakini Kabrass alijikakamua kutoka nyuma huku Matthias Osimbo, Fredrick Wangila, Brian Lukusi na Jackson Siketi wakipata touch down ili kukamilisha ushindi. Wakati huo huo, Mwamba Ladies waliishinda Kenya Harlequins 10-7 na kutwaa ubingwa wa wanawake. Kabrass alirudi nyumbani na kitita cha ksh 150,000 huku Mwamba ladies wakipata ksh 100,000 kwa hisani ya sportpesa.
Licha ya msimu wa 2026/27 wa KPL ukiwa wiki tatu tu kabla ya kuanza, mechi za kwanza bado hazina uhakika wa kuchezwa huku migogoro mingi ya kisheria ikiwa bado haijatatuliwa. Kesi mbili zinasubiriwa katika Mahakama Kuu ya Murang'a na nyingine mbele ya mahakama ya migogoro ya Michezo inayopinga sheria za kupanda na kushushwa daraja za FKF za 2025. Mahakama Kuu ya Murang'a itasikiliza ombi la kudharauliwa kwa mahakama dhidi ya Rais wa FKF Hussein Mohammed mnamo tarehe 14 mwezi huu, wiki moja tu kabla ya kuanza kwa mechi. Timu zote 18 ziko gizani na kuacha msimu mpya ukiwa katika sintofahamu kubwa.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Kisii, Kitale na Kericho.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.