Kocha mkuu wa timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Algeria, Farid Benstati, anatarajia mechi ngumu dhidi ya Harambee Starlets, katika pambano lao la mwisho la WAFCON usiku wa leo. Algeria wako katika nafasi ya pili katika kundi A wakiwa na pointi tatu nyuma ya wenyeji Morocco na wanahitaji angalau sare dhidi ya Starlets ili kufuzu kwa robo fainali. Benstati ambaye hivi karibuni amekabiliana na Kenya mara mbili anaamini wako tayari kwa pambano hilo. Mechi hiyo itaanza saa tano usiku, sawa na Morocco dhidi ya Senegal.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nanyuki, Meru na Isiolo.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.