Klabu ya KPL Nairobi United imemsajili mchezaji wa kimataifa wa Kongo Harvy Ossété kutoka klabu ya Libya Al-Dhahra SC. United iliwashinda miamba wa Sudan Al Hilal na vilabu vingine vya Afrika na kumsajili kiungo huyo. Mchezaji huyo wa zamani wa St-Éloi Lupopo aliwasili Nairobi jana, na atajiunga na wenzake wapya jijini Kampala Uganda kwa mechi zao za kirafiki za maandalizi ya msimu. Anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa wa hadhi kubwa baada ya makipa wa kimataifa wa Kenya Farouk Shikhalo na Gad Mathews kusajiliwa kutoka Ethiopian Coffee na Gor Mahia mtawalia.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Machakos, Kibwezi na Kitui.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.