ODM imesisitiza kwamba itaunga mkono ushirikiano na UDA katika Uchaguzi Mkuu wa 2027 ikiwa tu itapata nafasi ya mgombea mwenza wa naibu rais. Akizungumza jana, Katibu Mkuu wa ODM Catherine Omanyo alisema nafasi hiyo lazima iende kwa mwanachama halali wa ODM. Matamshi yake yalikuja baada ya Waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku kupendekeza kwamba Naibu Rais Kithure Kindiki anaweza hata kujiunga na ODM, mradi aendelee kuwa mgombea mwenza.


CATHERINE OMANYO-TUNATAKA