Wapelelezi wamemkamata Mbunge wa Mukurweini, John Kaguchia leo asubuhi nje ya studio za Royal Media Services jijini Nairobi baada ya kulala ndani ya jumba hilo. Mbunge huyo alidai polisi walikuwa wakimsubiri kumkamata kutokana na matamshi tata ya kisiasa aliyotoa wakati wa mahojiano ya televisheni. Kukamatwa huko kunafuatia ukosoaji mkubwa wa matamshi aliyoyatoa mbunge huyo ambapo inadaiwa aliwatishia wafuasi wa kisiasa wa Rais William Ruto kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027.