Familia na marafiki wa marehemu Benson Njiru na Emmanuel Mutura, maarufu kama ndugu wa Kianjakoma waliofariki mwaka wa 2021, wanatoa wito wa kuharakishwa kwa kesi hiyo. Wakizungumza wakati wa kumbukumbu ya miaka mitano tangu ndugu hao walipofariki wakiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kudaiwa kukiuka sheria za kutotoka nje za COVID-19, familia hiyo ilisema kasi ndogo ya kesi hiyo imeongeza maumivu yao na kuwanyima haki. Maafisa sita wa polisi wanahusishwa na kesi hiyo.
VOX POP-CASE