Wauguzi katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta  KNH leo wanatarajiwa kujiunga na wenzao katika mgomo na kuacha huduma za afya katika kaunti zisizopungua 20 zikiwa zimelemazwa. Kususia kazi kumezidisha mgogoro wa kiafya ambao tayari umesababishwa na mgomo unaoendelea wa wafanyakazi wa UHC. Kaunti zilizoathiriwa ni pamoja na Embu, Kitui, Samburu, Wajir, miongoni mwa zingine.