Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang'ula amewatetea Wakenya wenye asili ya Kihindi, akisisitiza kuwa wao ni raia sawa ambao haki zao lazima ziheshimiwe. Akizungumza bungeni, Wetang'ula aliwaonya viongozi dhidi ya kuchafua na kubaguana kikabila, akisema hakuna Mkenya anayepaswa kulengwa kwa sababu ya jamii yao. Aliwasihi viongozi kukuza umoja wa kitaifa na kuonya kwamba matamshi ya mgawanyiko yanaweza kudhoofisha mshikamano wa nchi.
MOSES WETANGULA - INDIANS