Viongozi katika eneo bunge la Rabai, Kaunti ya Kilifi, wamewahimiza wakaazi wanaostahili ambao bado hawajajiandikisha kama wapiga kura kufanya hivyo kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027. Wakiongozwa na Mbunge wa Rabai Antony Kenga, viongozi hao walisema zaidi ya wakaazi elfu 26 wenye vitambulisho vya kitaifa bado hawajajiandikisha kupiga kura. Kenga alisema ofisi yake, kwa ushirikiano na wasimamizi wa mashinani, imezindua kampeni ya uhamasishaji wa usajili wa wapiga kura.


ANTONY KENGA – VOTERS