Mswada wa Marekebisho wa Michezo wa Mbunge Irene Mayaka, mwaka 2026 umepita kusomwa kwa mara ya Pili katika Bunge la Kitaifa, na kuileta Kenya hatua karibu na kuanzisha sheria kali dhidi ya upangaji wa matokeo na udanganyifu wa Michezo. Muswada huo unalenga kurekebisha Sheria ya Michezo kwa mfumo wazi wa kuchunguza na kuadhibu vitendo vinavyodhoofisha uadilifu wa mashindano. Muswada huo pia unaanzisha kosa jipya chini ya Sheria ya Michezo, huku watu binafsi wakipatikana na hatia wakikabiliwa na kifungo cha hadi mwaka mmoja jela, faini ya hadi KSh1 milioni, au vyote viwili.


AFC Leopards wanatarajiwa kuelekea Tanzania kwa awamu ya mwisho ya maandalizi yao ya msimu wa maandalizi, huku msururu wa mechi za kirafiki zikiwa zimepangwa huku wakiimarisha kikosi chao kabla ya kampeni mpya. Wakati huo huo, Nairobi United itaondoka kwenda Uganda leo kuendelea na maandalizi yao ya msimu mpya. Klabu hiyo imeandaa mechi kadhaa za kirafiki dhidi ya timu za Uganda.



Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Mombasa, Malindi na Garissa.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.