Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna amewasihi viongozi wa upinzani kuungana kufuatia mkutano wa mashauriano na kiongozi wa Wiper KalonzoMusyoka. Alisema Wakenya wanatarajia viongozi wenye maadili ya pamoja kushirikiana katika kuendeleza utawala bora, uhuru wa kikatiba na haki za raia. Sifuna alibaini kuwa mazungumzo hayo yanalenga kujenga makubaliano na kuunda upinzani imara na wenye umoja kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027.

EDWIN SIFUNA - UNITY