Chama cha Mashujaa wa Vita vya Mau Mau kimeihimiza serikali kukabidhi Bustani ya Uhuru kwa Baraza la Kitaifa la Mashujaa kama ukumbusho na mahali pa kuzikwa kwa wapiganaji wa uhuru wa Kenya na watu mashuhuri wa kitaifa. Katibu Mkuu Gituwa Kahengeri alitoa wito huo baada ya kuwakaribisha maafisa wa baraza hilo nyumbani kwake Kilimambogo huko Kiambu. Pia alilihimiza baraza hilo kuweka mnara huko Shakahola katika Kaunti ya Kilifi kwa heshima ya mpiganaji wa uhuru Mekatilili wa Menza.
CHARLES WAMBIA - CHALLENGE