Polisi mjini Kisumu wanachunguza mauaji ya mfanyakazi wa kiwanda cha posho aliyepatikana amefariki ndani ya nyumba yake ya kupangisha huko Mamboleo, Kajulu. Wapelelezi wanasema mshukiwa aliacha ujumbe ulioandikwa kwa mkono akidai alimuua mwathiriwa kwa madai ya uhusiano wa kimapenzi unaomhusisha mkewe. Mwili wa mwathiriwa uligunduliwa ndani ya nyumba hiyo huku maafisa wakianzisha msako wa kumtafuta mshukiwa.