Baraza la Magavana linapanga kuwasilisha kesi mahakamani ili mgomo wa wauguzi unaoendelea utangazwe kuwa kinyume cha sheria. Mwenyekiti wa Kamati ya Afya ya COG Abdulswamad Nassir anasema matakwa muhimu, ikiwa ni pamoja na mazungumzo ya CBA na miongozo ya maendeleo ya kazi, tayari yanashughulikiwa, na kwamba baadhi ya matakwa hayo hayana msingi. Kisha anaongeza kwamba ingawa wauguzi wana haki ya kugoma, ustawi wa wagonjwa lazima pia ulindwe.


ABDULSWAMAD NASSIR –COURT