KWS imeiomba Bodi ya Bidhaa za Kudhibiti Wadudu (PCPB) kuchunguza mashamba yanayoshukiwa kutumia dawa za kuua wadudu zinazohusishwa na sumu ya cyanide kufuatia vifo vya ndovu 15 katika mfumo ikolojia wa Amboseli. Mkurugenzi Mkuu wa KWS Erustus Kanga alisema uchunguzi wa mashirika mengi umeombwa ili kufuatilia chanzo cha sumu hiyo na kubaini waliohusika. Matokeo ya awali yanaonyesha ndovu hao walikufa baada ya kumeza kemikali zenye sumu zinazoaminika kuwa zilitokana na dawa za kuua wadudu zinazotumika katika mashamba ya nyanya yaliyo karibu.