Naibu Rais Kithure Kindiki asubuhi ya leo ameondoka kuelekea Uganda kuhudhuria Mkutano mkuu wa Pili wa Ujumbe wa Usaidizi na Utulivu wa Umoja wa Afrika nchini Somalia (AUSSOM). Aliandamana na Waziri wa Ulinzi Soipan Tuya miongoni mwa maafisa wengine wa ngazi za juu serikalini.