Serikali inatoa wito kwa jamii kusaidia kupambana na ongezeko la wizi wa punda kote nchini. Katibu wa Utawala katika Wizara ya usalama Beverly Opwora anasema wazee wa vijiji, kamati za Nyumba Kumi na timu za usalama za kaunti zitachukua jukumu kubwa katika ukusanyaji wa taarifa za kijasusi na kutoa tahadhari mapema. Pia aliwasihi waendesha mashtaka, Mahakama, KRA na mashirika ya mipakani kuimarisha utekelezaji na kukabiliana na makundi ya ulanguzi wa punda yanayovuka mipaka.


BEVERLY OPWORA - PROTECT