Gavana wa Taita Taveta, Andrew Mwadime, ametoa wito wa kutenga bajeti zaidi ili kushughulikia uhaba mkubwa wa maji, ambao anautambua kama chanzo kikuu cha migogoro kati ya binadamu na wanyamapori katika eneo hilo. Akizungumza katika Hifadhi ya Kitaifa ya Tsavo Magharibi ambapo alijiunga na KWS kuadhimisha Siku ya Rangers Duniani, Mwadime alisisitiza kwamba eneo hilo linakabiliwa na uhaba wa maji na visima vilivyo na madini, akihimiza ufadhili zaidi wa kifedha kwa ajili ya maji ya bomba kwa wanyamapori wa eneo hilo na wakaazi.
ANDREW MWADIME – BUDGET