Watu wawili wamekamatwa kuhusiana na mauaji ya mtafiti wa afya ya akili Dkt. Victoria Mutiso huko Upper Hill jijini Nairobi. DCI inasema washukiwa wako kizuizini kisheria na wanahojiwa huku uchunguzi ukiendelea. Wapepelezi pia wamefanikiwa kupata vielelezo kutoka katika majengo yanayohusishwa na washukiwa, huku uchambuzi wa kisayansi ukiendelea. DCI inasema uchunguzi zaidi unafanywa ili kubaini mazingira yanayozunguka mauaji hayo.