Walimu wakuu wa shule wana hadi mwisho wa leo kuthibitisha kwamba alama za tathmini ya shule (SBA) kwa watahiniwa wa KPSEA na KJSEA mwaka huu zimenakiliwa kwa usahihi kwenye jukwaa la Baraza la Mitihani la Kitaifa KNEC. Zoezi hilo la uthibitishaji linalenga kuhakikisha kwamba alama zote za tathmini endelevu zimewekwa kwa usahihi na kuonyeshwa katika jukwaa la CBA kabla ya tathmini za kitaifa za mwaka huu.