Serikali imeongeza juhudi za kuimarisha usalama wa jamii, kupunguza biashara haramu ya dawa za kulevya na kuboresha upatikanaji wa huduma. Akizungumza mjini Mombasa, Katibu wa usalama Raymond Omollo alisema jukumu la kaunti hiyo kama lango kuu la Kenya kupitia Bandari ya Mombasa hufanya usalama wake kuwa muhimu kwa ukuaji wa uchumi, utalii, biashara na uwekezaji. Aliwaagiza Makamishna wa Kaunti na maafisa wa utawala kufanya kazi kwa karibu na mashirika ya usalama na jamii ili kupambana na uhalifu uliopangwa, magenge, msimamo mikali na ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya.

RAYMOND OMOLLO - FIND