Naibu Kiongozi wa Chama cha Safina Willis Otieno amekosoa Muswada wa Sheria za Uchaguzi (Marekebisho), 2026 unaolenga kuondoa sharti la kisheria kwa IEBC kupeperusha moja kwa moja matokeo ya uchaguzi kutoka vituo vya kupigia kura, akionya kwamba mabadiliko hayo yanaweza kudhoofisha uwazi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027. Wakili huyo kupitia akaunti yake ya X alisema kuondoa sharti hilo kutawanyima Wakenya fursa ya kwanza ya kuthibitisha matokeo ya uchaguzi kwa uhuru yanapotangazwa kote nchini.