Serikali ya Kaunti ya Kirinyaga inajenga vituo vinne vipya vya kununulia chai ili kuwasaidia wakulima kupunguza hasara baada ya mavuno kwa majani ya chai yaliyovunwa hivi karibuni katika kata za Inooi na Kerugoya. Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru anasema vituo hivyo vipya vitahudumia wakulima wadogo wapatao 800 wa chai katika wasi ya Kerugoya na takriban wakulima elfu moja katika wadi ya Inooi. Vituo vya kununulia chai hutumika kama sehemu ya kwanza ya ukusanyaji, ambapo majani ya chai yaliyovunwa hivi karibuni huwasilishwa, hupimwa na kurekodiwa kabla ya kusafirishwa hadi viwandani kwa ajili ya kusindika.