Baraza la Kitaifa la Utawala wa Haki limewahakikishia Wakenya kwamba hakuna mgogoro katika sekta ya haki, likisema taasisi zinaendelea kufanya kazi kwa karibu ili kuboresha utoaji wa huduma. Katika taarifa iliyotolewa baada ya mkutano wake wa 38, Baraza hilo lilisema shughuli zake zinasalia kuratibiwa vizuri kupitia miundo ya kitaifa na ya mashinani, ikiwa ni pamoja na Kamati za Watumiaji wa Mahakama, ili kuimarisha upatikanaji wa haki na kushughulikia changamoto zinazowaathiri watafutaji haki.
MARTHA KOOME - DISMISS