Waziri wa ICT William Kabogo na mwenzake wa Michezo Salim Mvurya wanatarajiwa kufika mbele ya Kikao cha Bunge la Seneti kujibu maswali kutoka kwa maseneta. Waziri Kabogo anatarajiwa kuangazia hatua zilizowekwa na Serikali kushughulikia usambazaji wa taarifa za dharura za uongo, maudhui yaliyobadilishwa kidijitali na kuigwa kwa taasisi za umma au maafisa mtandaoni.