Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna na mwenzake wa Vihiga Godffrey Osotsi wameondolewa kutoka kwa kamati mbili za ufuatiliaji zenye ushawishi mkubwa katika Seneti. Sifuna ameondolewa kutoka kwa kamati ya fedha  za Umma za Kaunti huku Osotsi akipoteza nafasi yake kama mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji wa Umma wa Kaunti na Fedha Maalum. Hii ni kubanduliwa kwa mwisho kisiasa kunakowalenga wakosoaji wa serikali pana.