Muswada unaolenga kurekebisha Katiba ili kufikia kanuni ya jinsia ya theluthi mbili na kuboresha uwakilishi kwa watu wenye ulemavu unatarajiwa kuwasilishwa katika Bunge la Kitaifa hii leo. Muswada huo wa wabunge Gladys Boss, Beatrice Elachi na Jane Kagiri unapendekeza kuundwa kwa viti maalum Bungeni ili wabunge wasiozidi theluthi mbili wawe wa jinsia moja.