KWS  imeanzisha uchunguzi wa kina kufuatia vifo vya ndovu 15 katika mfumo ikolojia wa Amboseli kwa kipindi cha mwezi mmoja. Matokeo ya awali yanaonyesha sumu inayowezekana huku wataalamu wakifanya kazi ili kubaini chanzo halisi. KWS ilisema vifo vya ndovu vilirekodiwa kati ya Juni tarehe 24 na Julai tarehe 24, katika Hifadhi ya Kitaifa ya Amboseli. Inasema 10 kati ndovu hao walionyesha dalili za kufanana kabla ya kufa.